Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. 1Njoni, mtukuzeni Yahwe, enyi nyote watumishi wa Yahwe, ninyi mnaotumika hekaluni mwa Yahwe wakati wa usiku. 2Inueni mikono yenu patakatifu pake na mtukuzeni Yahwe. 3Mungu na awabariki toka Sayuni, yeye aliye ziumba mbingu na nchi.