Kwa kiongozi wa muziki. Maschil ya Daudi; wakati Doegi Mwedomi alipokuja na kumwambia Sauli, na kumwambia yeye, “Daudi amekuja kwenye nyumba ya Ahimeleki.” 1Kwa nini wewe unajivunia kufanya uovu, wewe mtu mwenye nguvu? Uaminifu wa agano la Mungu huja kila siku. 2Ulimi wako hupanga uharibifu kama wembe mkali, na kufanya udanganyifu. 3Wewe unapenda uovu kuliko wema na udanganifu kuliko kuongea haki. Selah 4Wewe hupenda maneno ambayo huwaumiza wengine, wewe ulimi mdanganyifu. 5Vivyo hivyo Mungu atakuadhibu wewe milele; yeye atakuchukua na kukuondoa katika hema yako na kukung'oa katika ardhi ya uhai. Selah 6Wenye haki pia wataona na kuogopa; watamcheka na kusema, 7“Tazama, huyu ni mtu ambaye hakumfanya Mungu kuwa kimbilio lake la usalama, bali aliamini katika wingi wa mali zake, naye alikuwa na nguvu alipowaharibu wengine.” 8Lakini kwangu mimi, niko kama mti bora wa mzeituni katika nyumba ya Mungu; Nami nitaamini uaminifu wa agano la Mungu milele na milele. 9Nitakushukuru wewe daima kwa uliyo tenda. Nitalisubiri jina lako, kwa sababu ni zuri, uweponi mwa wantu wako wa kimungu.