Zaburi ya Daudi, wakati alipo mkimbia mtoto wake Absalom. 1Yahewh, maadui zangu wako wangapi! Ni wengi wamekuja kinyume na mimi. 2Ni wengi wanaonisema, “Hakuna msaada wowote kutoka kwa Mungu kwa ajili yake.” Selah 3Bali wewe, Yahweh, u ngao yangu pande zote, utukufu wangu, na uniinuaye kichwa changu. 4Nampazia Yahweh sauti yangu, na yeye ananijibu kutoka katika mlima wake mtakatifu. 5Nilijilaza chini na kusinzia; na niliamka, kwa kuwa Yahweh alinilinda. 6Sitaogopa kusanyiko la watu ambao wamejipanga kinyume na mimi pande zote. 7Inuka, Yahweh! Uniokoe, Mungu wangu! Kwa kuwa utawapiga maadui zangu wote kwenye taya zao; utayavunja meno ya waovu. 8Wokovu unatoka kwa Yahweh. Baraka zako ziwe juu ya watu wako.