Zaburi ya wana wa Kora; wimbo. 1Mji aliouanzisha umesimama juu ya mlima mtakatifu; 2Yahwe anapenda zaidi malango ya Sayuni kuliko mahema yote ya Yakobo. 3Mambo matukufu yamesemwa kwako, mji wa Mungu. Selah 4Ninataja Rahabu na Babeli kwa wafuasi wangu. Tazama, Filisti, na Tiro, pamoja na Ethiopia nao watasema, 'Huyu alizaliwa humo.'” 5Itasemwa juu ya Sayuni, “Kila mmoja wa hawa alizaliwa katika yeye; na yeye Aliye Juu atamuimarisha. 6Yahwe anaandika katika kitabau cha sensa ya mataifa, “Huyu alizaliwa humo.” Selah 7Hivyo waimbaji na wachezaji kwa pamoja waseme, “chemchem zangu zimo kwako.”