Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. 1Amebarikiwa kila mtu amchaye Yahwe, atembeaye katika njia zake. 2Kazi ya mikono yako, wewe utaifurahia; utabarikiwa na kufanikiwa. 3Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao katika nyumba yako; wanao watakuwa kama miche ya mimea ya mizeituni wakaapo kuzunguka meza yako. 4Ndiyo, hakika, mtu anaye muheshimu Yahwe atabarikiwa. 5Mungu na akubariki toka Sayuni; na uweze kuona mafanikio ya Yerusalemu siku zote za maisha yako. 6Uishi uwaone wana wa wanao. Amani iwe na Israli.