1Israeli ilipotoka Misri, na nyumba ya Yakobo toka kutoka katika wale watu wa kigeni, 2Yuda ilifanyika kuwa mahali pake patakatifu, Ufalme wa Israeli. 3Bahari iliona ikakimbia; Yordani ilirudi nyuma. 4Milima iliruka kama kondoo waume, vilima viliruka kama wana-kondoo. 5Ewe Bahari kwa nini ulikimbia? Yordani kwa nini ulirudi nyuma? 6Milima, kwa nini uliruka kama kondoo waume? Enyi vilima wadogo, kwa nini mliruka kama wana-kondoo? 7Tetemeka, ee nchi, mbele za Bwana, uweponi mwa Mungu wa Yakobo. 8Aligeuza mwamba kuwa ziwa la maji, jiwe gumu kuwa chemchem.