Zaburi ya Daudi. 1Yahwe humwambia bwana wangu, “Kaa mkono wangu wa kuume mpaka nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.” 2Yahwe atainyosha fimbo ya nguvu yako toka Sayuni; utawale kati ya adui zako. 3Siku ile ya uweza wako watu wako watakufuata wakiwa katika mavazi matakatifu ya hiari yao wenyewe; tokea tumbo la alfajiri ujana wako utakuwa kwako kama umande. 4Yahwe ameapa, na hatabadilika: “Wewe ni kuhani milele, baada ya namna ya Melkizedeki.” 5Bwana yuko mkono wako wa kuume. Siku ile ya hasira yake atawaua wafalme. 6Yeye atahukumu matifa; ataujaza uwanja wa vita kwa maiti; atawauwa viongozi kaitka nchi nyingi. 7Atakunywa maji ya kijito njiani, kisha baada ya ushindi atainua kichwa chake juu.