1Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Bado kuna pigo moja nitalo lileta kwa Farao na Misri. Baada ya hilo, atakuacha uondoke hapa. Atakapo kuachia uende, ata kuondoa kabisa. 2Waelekeze watu kwamba kila mwanaume na mwanamke amuulizie jirani yake vitu vya fedha na vitu vya dhahabu.” 3Sasa Yahweh aliwafanya Wamisri kuwa na shauku ya kuwapendeza Waisraeli. Aidha, Musa alikuwa wakuvutia sana machoni pa watumishi wa Farao na watu wa Misri. 4Musa akasema, “Yahweh asema hivi: 'Wakati wa usiku wa manane nitaenda Misri yote. 5Wazaliwa wa kwanza wote wa nchi ya Misri watakufa, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, anaye keti kiti chake cha enzi, mpaka mzaliwa wa kwanza wa misichana mtumwa anaye saga mbegu, na kwa wazaliwa wa kwanza wa mifugo. 6Kisha kutakuwa na kilio kikubwa nchi yote ya Misri, kama ambacho hakijawai wala hakitatokea tena. 7Lakini ata mbwa hata bweka kwa watu wa Israeli, dhidi ya mtu au mnyama. Kwa hili utajuwa kuwa nina watendea Wamisri na Waisraeli tofauti.' 8Watumishi wote hawa wako, Farao, watakuja chini yangu na kunisujudu mimi. Watasema, 'Nenda, wewe na watu wote wanao kufuata!' Baada ya hapo nitaondoka.” Kisha akaondoka mbele ya Farao kwa hasira kubwa. 9Yahweh akamwambia Musa, Farao hatakusikiliza. Hii ni ili nifanye mambo ya ajabu katika nchi ya Misri.” 10Musa na Aruni wakafanya mambo haya ya kushangaza mbele za Farao. Lakini Yahweh aliufanya moyo wa Farao mgumu, na Farao hakuwaacha watu wa Israeli kuondoka katika nchi yake.