1Baada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na nikaweka milango, mabawabu wa lango, waimbaji, na Walawi waliteuliwa. 2Nikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine. 3Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”
Orodha Ya Waliorudi Toka Uhamishoni
(Ezra 2:1-70)
4Mji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu. 5Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu wa kawaida kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndiyo niliyokuta yameandikwa humo:
6Hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, 7wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispereti, Bigwai, Nehumu na Baana):
Orodha ya wanaume wa Israeli ilikuwa:
39Makuhani:
43Walawi:
44Waimbaji:
45Mabawabu wa malango:
46Watumishi wa Hekalu:
wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,
47wazao wa Kerosi, Sia, Padoni,
48wazao wa Lebana, Hagaba, Shalmai,
49wazao wa Hanani, Gideli, Gahari,
50wazao wa Reaya, Resini, Nekoda,
51wazao wa Gazamu, Uza, Pasea,
52wazao wa Besai, Meunimu, Nefusimu,
53wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
54wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
55wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
56wazao wa Nesia na Hatifa.
57Wazao wa watumishi wa Solomoni:
wazao wa Sotai, Soferethi, Perida,
58wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,
59wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Amoni.
61Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
63Na kutoka miongoni mwa makuhani:
wazao wa Hobaya, Hakosi na Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).
64Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 65Kwa hiyo, mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.
66Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; 67tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 245. 68Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245 69ngamia 435 na punda 6,720.
70Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,000 za dhahabu, mabakuli 50, na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani. 71Baadhi ya viongozi wa jamaa walikabidhi kwenye hazina darkoni 20,000 za dhahabu, na mane 2,200 za fedha kwa ajili ya kazi hiyo.
72Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni 20,000 za dhahabu, mane 2,000 za fedha, na mavazi sitini na saba ya makuhani.
73Makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji na watumishi wa Hekalu, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao wenyewe.
Ezra Asoma Sheria
Ilipotimia miezi saba, nao Waisraeli wakiwa tayari wanaishi katika miji yao,

Notes


*7:46 Yaani Wanethini (pia 7:60, 73).

7:65 Au Tirshatha: jina la heshima aliloitwa mtawala wa Yuda chini ya Ufalme wa Uajemi (pia 7:70).

7:65 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.

§7:70 Darkoni 1,000 za dhahabu ni sawa na uzito wa kilo 8.6.

*7:71 Darkoni 20,000 za dhahabu ni sawa na kilo 172.

7:71 Mane 2,200 za fedha ni sawa na kilo 1,300.